Skip to content
النِّسَاء /

Aya 15

4 : 15

Aya 15 of النِّسَاء (4 : 15). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 15

وَٱلَّٰتِي يَأۡتِينَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مِن نِّسَآئِكُمۡ فَٱسۡتَشۡهِدُواْ عَلَيۡهِنَّ أَرۡبَعَةٗ مِّنكُمۡۖ فَإِن شَهِدُواْ فَأَمۡسِكُوهُنَّ فِي ٱلۡبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّىٰهُنَّ ٱلۡمَوۡتُ أَوۡ يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لَهُنَّ سَبِيلٗا

Na ambao wanafanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, washuhudizieni watu wane katika nyinyi. Watakapo shuhudia, basi wazuieni majumbani mpaka wafishwe na mauti au Mwenyezi Mungu awatolee njia nyengine.

Explanation & meanings · 1
  1. Na wale wanawake wanao zini wakishuhudiwa na mashahidi wanaume wane walio waadilifu, basi wazuieni wasitoke nyumbani kwa ajili ya kuwalinda na kuzuia usiendelee ufisadi na shari mpaka wafe, au Mwenyezi Mungu awafungulie njia ya maisha yaliyo sawa kwa kuolewa na kutubu. (Wafasiri wengine wanasema hukumu hii ni kwa wanawake wanao fanya mambo machafu wenyewe kwa wenyewe, sio ya zina baina ya mwanamke na mwanamume. Kwa kuhifadhi heshima ya wanawake inalazimu wapatikane mashahidi wane, badala ya wawili, walio ona kitendo khasa, sio kuwatuhumu watu kwa jambo ovu kama hilo bila ya mashahidi wane walio shuhudia kwa macho yao.)