Skip to content
النِّسَاء /

Aya 149

4 : 149
النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 149

إِن تُبۡدُواْ خَيۡرًا أَوۡ تُخۡفُوهُ أَوۡ تَعۡفُواْ عَن سُوٓءٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوّٗا قَدِيرًا

Mkidhihirisha wema au mkiuficha, au mkiyasamehe maovu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Muweza.

Explanation & meanings · 1
  1. Mkiyadhihirisha mema myatendayo, au mkayaficha, au mkamsamehe anaye kufanyieni uovu, Mwenyezi Mungu atakulipeni kwa kufuata khulka yake Mtukufu, ya kusamehe na hali ana uwezo kaamili. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni mwingi mno wa kusamehe, Mwenye kukamilika uwezo wake.