Skip to content
النِّسَاء /

Aya 139

4 : 139
النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 139

ٱلَّذِينَ يَتَّخِذُونَ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَيَبۡتَغُونَ عِندَهُمُ ٱلۡعِزَّةَ فَإِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعٗا

Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.

Explanation & meanings · 1
  1. Hao wanaafiki huufanya utawala wa makafiri uwe juu yao, na wanawawacha Waumini. Basi hebu hivyo wanataka wapate utukufu kwa hawa makafiri? Hakika utukufu uko kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye huwapa waja wake wenye kuamini. Na mwenye kutaka utukufu kwa Mwenyezi Mungu atatukuka, na mwenye kutaka utukufu kwa mwenginewe atadhalilika.