Skip to content
النِّسَاء /

Aya 114

4 : 114

Aya 114 of النِّسَاء (4 : 114). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 114

۞ لَّا خَيۡرَ فِي كَثِيرٖ مِّن نَّجۡوَىٰهُمۡ إِلَّا مَنۡ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوۡ مَعۡرُوفٍ أَوۡ إِصۡلَٰحِۭ بَيۡنَ ٱلنَّاسِۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِ فَسَوۡفَ نُؤۡتِيهِ أَجۡرًا عَظِيمٗا

Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika wale wanao kaa wakipanga mambo yao kisirisiri, mambo hayo hayana kheri, kwa sababu shari ndio huchipuka katika ufichoni. Lakini ikiwa mazungumzo hayo ni kwa jambo la sadaka ya kuwapa watu, au kufanya jambo lolote lisio baya, au kupanga mipango ya kusuluhisha baina ya watu, hayo si mabaya. Kwani hayo ni mambo ya kheri. Na mwenye kufanya hivyo kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Subhanahu Wataa'la, basi Mwenyezi Mungu atampa malipo makubwa duniani na Akhera.