4 : 106
وَٱسۡتَغۡفِرِ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na muombe maghfira Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu.
Explanation & meanings · 1
- Na unapo hukumu baina ya watu muelekee Mwenyezi Mungu, na ukumbuke utukufu wake, na uombe maghfira yake na rehema yake. Kwani kughufiria na kurehemu ndio shani yake Subhanahu wa Taa'la.