Skip to content
فَاطِر /

Aya 40

35 : 40

Aya 40 of فَاطِر (35 : 40). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

فَاطِر Aya 45
Sura · فَاطِر
Kiswahili · Barawani
35 : 40

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ شُرَكَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُواْ مِنَ ٱلۡأَرۡضِ أَمۡ لَهُمۡ شِرۡكٞ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ أَمۡ ءَاتَيۡنَٰهُمۡ كِتَٰبٗا فَهُمۡ عَلَىٰ بَيِّنَتٖ مِّنۡهُۚ بَلۡ إِن يَعِدُ ٱلظَّٰلِمُونَ بَعۡضُهُم بَعۡضًا إِلَّا غُرُورًا

Sema: Mnawaona hawa miungu wenu wa kishirikina mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu! Nionyesheni wameumba sehemu gani katika ardhi? Au wana ushirika wowote katika mbingu? Au tumewapa Kitabu nao kwa hicho wakawa na hoja zilizo wazi? Lakini madhaalimu hawaahidiani wao kwa wao ila udanganyifu tu.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Waambie washirikina: Hebu nambieni, mmeiona hali ya hawa miungu wenu wa kishirikina mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Hebu nambieni, sehemu gani katika ardhi waliyo iumba wao? Hebu wanao ushirika wowote na Mwenyezi Mungu katika kuziumba mbingu? Sisi hatukuwapa kitabu cha ushirikina wakawa wao wanatoa hoja kutoka humo. Lakini wenye kudhulumu hawaahidiani wenyewe kwa wenyewe kwa uombezi wa miungu yao ya kumshirikisha na Mwenyezi Mungu ila kwa uwongo na kupambia pambia kuso mdanganya mtu ila aliye kuwa akili yake ni dhaifu.