Skip to content
الأحزَاب /

Aya 52

33 : 52

Aya 52 of الأحزَاب (33 : 52). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأحزَاب Aya 73
Sura · الأحزَاب
Kiswahili · Barawani
33 : 52

لَّا يَحِلُّ لَكَ ٱلنِّسَآءُ مِنۢ بَعۡدُ وَلَآ أَن تَبَدَّلَ بِهِنَّ مِنۡ أَزۡوَٰجٖ وَلَوۡ أَعۡجَبَكَ حُسۡنُهُنَّ إِلَّا مَا مَلَكَتۡ يَمِينُكَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ رَّقِيبٗا

Baada ya hawa hawakuhalalikii wewe wanawake wengine, wala kuwabadilisha kwa wake wengine ingawa uzuri wao ukikupendeza; isipo kuwa yule uliye mmiliki kwa mkono wako wa kulia. Na Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu.

Explanation & meanings · 1
  1. Hawakuhalalikii wanawake wengine baada ya hawa, wala kuwapa t'alaka kwa ajili ya kuwabadilisha kwa wengine uwatakao, hata wakikupendeza kwa uzuri wao. Lakini Mwenyezi Mungu amekuhalalishia wajakazi ulio wamiliki kwa mkono wako. Na Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu, na anakihifadhi.