Skip to content
الأحزَاب /

Aya 22

33 : 22

Aya 22 of الأحزَاب (33 : 22). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأحزَاب Aya 73
Sura · الأحزَاب
Kiswahili · Barawani
33 : 22

وَلَمَّا رَءَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلۡأَحۡزَابَ قَالُواْ هَٰذَا مَا وَعَدَنَا ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَصَدَقَ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥۚ وَمَا زَادَهُمۡ إِلَّآ إِيمَٰنٗا وَتَسۡلِيمٗا

Na Waumini walipo yaona makundi, walisema: Haya ndiyo aliyo tuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli. Na hayo hayakuwazidisha ila Imani na ut'iifu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na Waumini walipo yaona makundi ya washirikina walisema: Haya ndiyo aliyo tuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake zamani. Kwani walituahidi tutapata shida, na kisha tutapata ushindi. Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli. Taabu hizi basi, hazikuwazidishia ila nguvu za kumuamini Mwenyezi Mungu, na uzuri wa kuinyenyekea kwao hukumu yake.