28 : 12
۞ وَحَرَّمۡنَا عَلَيۡهِ ٱلۡمَرَاضِعَ مِن قَبۡلُ فَقَالَتۡ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰٓ أَهۡلِ بَيۡتٖ يَكۡفُلُونَهُۥ لَكُمۡ وَهُمۡ لَهُۥ نَٰصِحُونَ
Na tukamjaalia awakatae wanyonyeshaji wote tangu mwanzo, mpaka dada yake akasema: Je! Nikuonyesheni watu wa nyumba watakao mlea kwa ajili yenu, nao pia watakuwa wema kwake?
Explanation & meanings · 1
- Mwenyezi Mungu alimjaalia yule mtoto akatae ziwa la kila mnyonyeshaji kabla hawajamjia mama yake. Watu wa Firauni wakaingiwa na ghamu, na wakashughulishwa na hayo. Yule dada yake ndio akawaambia: Nikuongozeni kwenye ukoo utakao muangalia huyu mtoto, na kumnyonyesha, na kumlea, nao watamtazama vizuri?