Skip to content
النور /

Aya 37

24 : 37

Aya 37 of النور (24 : 37). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النور Aya 64
Sura · النور
Kiswahili · Barawani
24 : 37

رِجَالٞ لَّا تُلۡهِيهِمۡ تِجَٰرَةٞ وَلَا بَيۡعٌ عَن ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَإِقَامِ ٱلصَّلَوٰةِ وَإِيتَآءِ ٱلزَّكَوٰةِ يَخَافُونَ يَوۡمٗا تَتَقَلَّبُ فِيهِ ٱلۡقُلُوبُ وَٱلۡأَبۡصَٰرُ

Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka.

Explanation & meanings · 1
  1. Dunia na yaliomo duniani ya kuuza na kununua hayawashughulishi wakaacha kumdhukuru Mwenyezi Mungu na kumzingatia. Wao wanashika Swala, na wanatoa Zaka, na huku wakiikhofu Siku ya Kiyama ambapo nyoyo zitakuwa hazina utulivu kwa sababu ya wasiwasi na hamu, na kungojea matokeo, na macho yatadahadari kwa mhangaiko na kushtuka kwa vituko vigeni wanavyo viona, na wingi wa vitisho.