22 : 12
يَدۡعُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُۥ وَمَا لَا يَنفَعُهُۥۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلضَّلَٰلُ ٱلۡبَعِيدُ
Badala ya Mwenyezi Mungu, yeye huomba kisicho mdhuru wala kumnufaisha. Huko ndiko kupotolea mbali!
Explanation & meanings · 1
- Mwenye kukhasiri hivi humuacha Mwenyezi Mungu na akayaabudu masanamu yasiyo weza kumdhuru pindi akito yaabudu, wala hayamfai kitu pindi akiyaabudu. Kitendo chake huyo ndio kupotelea mbali na haki na uwongofu.