Skip to content
الحج /

Aya 11

22 : 11

Aya 11 of الحج (22 : 11). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الحج Aya 78
Sura · الحج
Kiswahili · Barawani
22 : 11

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَعۡبُدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ حَرۡفٖۖ فَإِنۡ أَصَابَهُۥ خَيۡرٌ ٱطۡمَأَنَّ بِهِۦۖ وَإِنۡ أَصَابَتۡهُ فِتۡنَةٌ ٱنقَلَبَ عَلَىٰ وَجۡهِهِۦ خَسِرَ ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةَۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡخُسۡرَانُ ٱلۡمُبِينُ

Na katika watu wapo wanao muabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na Akhera; hiyo ndiyo khasara iliyo wazi.

Explanation & meanings · 1
  1. Na miongoni mwa watu wapo wa namna ya tatu, ambao Imani bado haijatulia katika nyoyo zao, bali itikadi yao inayumba yumba. Maslaha ya nafsi zao ndiyo yanatawala katika Imani yao. Wakipata kheri hufurahi na hutulizana. Na wakipata shida yoyote katika nafsi zao, au mali zao, au wana wao, hurejea ukafirini. Hao huwa wamekosa duniani raha ya utulivu kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na nusura yake, kama Akhera walivyo kosa neema ambayo Mwenyezi Mungu amewaahidi Waumini walio thibiti na wakasubiri. Hiyo khasara ya mara mbili ndiyo khasara ya kweli kweli iliyo wazi.