Skip to content
البَقَرَة /

Aya 71

2 : 71
البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 71

قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٞ لَّا ذَلُولٞ تُثِيرُ ٱلۡأَرۡضَ وَلَا تَسۡقِي ٱلۡحَرۡثَ مُسَلَّمَةٞ لَّا شِيَةَ فِيهَاۚ قَالُواْ ٱلۡـَٰٔنَ جِئۡتَ بِٱلۡحَقِّۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُواْ يَفۡعَلُونَ

Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo ni Ng'ombe asiye tiwa kazini kulima Ardhi wala kumwagia maji mimea, mzima, hana baka. Wakasema: Sasa umeleta haki. Basi wakamchinja, na walikaribia kuwa wasifanye hayo.

Explanation & meanings · 1
  1. Musa akawambia: Mwenyezi Mungu anasema kuwa Ng'ombe huyo bado hajatiwa kazini kwa kulima wala kumwagia maji shambani kwa ajili ya makulima. Naye hana ila yoyote, mzima kabisa, wala katika mwili wake hana kibaka chochote, wote ni wa rangi moja. Hapo tena wakamwambia: Sasa umepambanua vilivyo. Wakamtafuta Ng'ombe mwenye sifa hizo wakamchinja. Na walikuwa wamekaribia wasifanye hayo kwa kukithiri masuala yao na wingi wa kushikilia kwao.