Skip to content
البَقَرَة /

Aya 284

2 : 284

Aya 284 of البَقَرَة (2 : 284). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 284

لِّلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَإِن تُبۡدُواْ مَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ أَوۡ تُخۡفُوهُ يُحَاسِبۡكُم بِهِ ٱللَّهُۖ فَيَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Viliomo mbinguni na viliomo duniani ni vya Mwenyezi Mungu. Na mkidhihirisha yaliyomo katika nafsi zenu au mkayaficha, Mwenyezi Mungu atakuhisabuni kwayo. Kisha amsamehe amtakaye na amuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

Explanation & meanings · 1
  1. Jueni kuwa vyote viliomo mbinguni na duniani ni vya Mwenyezi Mungu, naye ana makdara navyo vyote na anavijua vyote. Ni sawa sawa ikiwa mtadhihirisha yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkificha, Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa vyote na mwenye kupata khabari za vyote. Naye Siku ya Kiyama atakuhisabuni kwa hayo, na atamghufiria amtakaye na atamuadhibu amtakaye. Yeye ni Muweza wa kila kitu.