Skip to content
البَقَرَة /

Aya 149

2 : 149

Aya 149 of البَقَرَة (2 : 149). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 149

وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۖ وَإِنَّهُۥ لَلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo ndiyo Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Basi katika Swala zako popote pale ulipo uelekee Msikiti Mtakatifu, ukiwa upo mjini au umo safarini, popote wendapo. Na hakika haya bila ya shaka ndiyo ya Haki yanayo wafikiana na hikima ya Mola wako Mlezi aliye pamoja nawe. Basi wewe na umma wako yatamanini haya. Kwani Mwenyezi Mungu atakulipeni malipo mema kabisa. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye ujuzi wala hapana katika vitendo vyenu vilivyo fichikana naye.