Skip to content
البَقَرَة /

Aya 139

2 : 139

Aya 139 of البَقَرَة (2 : 139). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 139

قُلۡ أَتُحَآجُّونَنَا فِي ٱللَّهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمۡ وَلَنَآ أَعۡمَٰلُنَا وَلَكُمۡ أَعۡمَٰلُكُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُخۡلِصُونَ

Sema: Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu, naye ni Mola wetu Mlezi na Mola wenu Mlezi, na sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu? Nasi tunamsafia Yeye tu.

Explanation & meanings · 1
  1. Waambieni: Mnajadiliana nasi katika mambo ya Mwenyezi Mungu mkidai kuwa Yeye hakuteuwa Manabii ila kutokana nanyi tu? Na Mwenyezi Mungu ni Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa kila kitu; hawapendelei kaumu fulani akawatupa wengine. Rehema yake humfikia amtakaye, na huwalipa watu wote kwa vitendo vyao, bila ya kuangalia nasaba yao na ukoo wao. Na Yeye ametuongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka katika vitendo vyetu. Na ameturuzuku tumsafie niya na vitendo Yeye.