Skip to content
البَقَرَة /

Aya 115

2 : 115

Aya 115 of البَقَرَة (2 : 115). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 115

وَلِلَّهِ ٱلۡمَشۡرِقُ وَٱلۡمَغۡرِبُۚ فَأَيۡنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجۡهُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ

Na mashariki na magharibi ni za Mwenyezi Mungu. Basi kokote mnako elekea, huko Mwenyezi Mungu yupo. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa na Mjuzi.

Explanation & meanings · 1
  1. Ikiwa washirikina waliwazuia Waislamu kusali katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, hawatoweza kuwazuia kusali na kumuabudu Mwenyezi Mungu. Kwani jiha zote na pande zote za dunia ni za Mwenyezi Mungu. Na hakika bila ya shaka Mwenyezi Mungu anampokelea Muislamu Sala zake, na anamkabili kwa radhi yake pande zote anapo fanya ibada yake. Kwani Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa, hawadhikishi waja wake, na Yeye ni Mwenye kuijua vyema niya ya mwenye kumuelekea.