Skip to content
البَقَرَة /

Aya 109

2 : 109

Aya 109 of البَقَرَة (2 : 109). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 109

وَدَّ كَثِيرٞ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَوۡ يَرُدُّونَكُم مِّنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِكُمۡ كُفَّارًا حَسَدٗا مِّنۡ عِندِ أَنفُسِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلۡحَقُّۖ فَٱعۡفُواْ وَٱصۡفَحُواْ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ ٱللَّهُ بِأَمۡرِهِۦٓۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki. Basi sameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atapo leta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na wengi miongoni mwa Mayahudi wametamani kukurejesheni, enyi Waislamu, kwenye ukafiri baada ya kuwa nyinyi mmekwisha amini. Na haya juu ya kuwa wao imekwisha wadhihirikia kutoka na hicho hicho Kitabu chao kuwa nyinyi mpo juu ya Haki. Na hayakuwa hayo ila ni kuwa wanakuhusuduni na wanaogopa utawala usiwatoke mikononi mwao mkapewa nyinyi. Basi nyinyi wapuuzeni, na wasameheni, na waachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu akuonyesheni lipi jengine la kuwafanyia, kwani Yeye ni Muweza wa kukupeni ushindi juu yao, na Yeye ni Muweza wa kila kitu.