Skip to content
الكَهف /

Aya 32

18 : 32

Aya 32 of الكَهف (18 : 32). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الكَهف Aya 110
Sura · الكَهف
Kiswahili · Barawani
18 : 32

۞ وَٱضۡرِبۡ لَهُم مَّثَلٗا رَّجُلَيۡنِ جَعَلۡنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيۡنِ مِنۡ أَعۡنَٰبٖ وَحَفَفۡنَٰهُمَا بِنَخۡلٖ وَجَعَلۡنَا بَيۡنَهُمَا زَرۡعٗا

Na wapigie mfano wa watu wawili: mmoja wao tulimpa vitalu viwili vya mizabibu, na tukavizungushia mitende, na kati yake tukatia mimea ya nafaka.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Mtume! Bainisha baina ya hali ya makafiri matajiri na Waumini mafakiri kwa kuwapigia mfano ulio tokea hapo zamani baina ya watu wawili: kafiri na Muumini. Huyo kafiri alikuwa na vitalu viwili vya mizabibu, na tukavizungushia mitende kwa ajili ya pambo na faida pia. Na baina ya hivyo vitalu tukaweka makulima mengine yaliyo stawi na kutoa mazao.