Skip to content
الكَهف /

Aya 31

18 : 31

Aya 31 of الكَهف (18 : 31). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الكَهف Aya 110
Sura · الكَهف
Kiswahili · Barawani
18 : 31

أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ جَنَّٰتُ عَدۡنٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمُ ٱلۡأَنۡهَٰرُ يُحَلَّوۡنَ فِيهَا مِنۡ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٖ وَيَلۡبَسُونَ ثِيَابًا خُضۡرٗا مِّن سُندُسٖ وَإِسۡتَبۡرَقٖ مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِۚ نِعۡمَ ٱلثَّوَابُ وَحَسُنَتۡ مُرۡتَفَقٗا

Hao watapata Bustani za milele, zinazo pita mito kati yake. Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri na at'ilasi, huku wakiegemea humo juu ya makochi. Ni malipo bora hayo! Na matandiko mazuri mno ya kupumzikia!

Explanation & meanings · 1
  1. Watu hao watakuwa na Mabustani ambayo watastarehe ndani yake daima dawamu. Kati baina ya miti na majumba yake inapita mito, na watapambiwa yanayo onekana ni ya starehe katika dunia, kama mapambo ya dhahabu, na mavazi yao ni nguo za kijani za hariri za kila namna, wakiegemea juu ya makochi na matakia na mapazia. Watapata malipo bora, na Bustani nzuri ya kudumu na kustarehe. Humo watapata kila wakitakacho.