Skip to content
الإسرَاء /

Aya 101

17 : 101

Aya 101 of الإسرَاء (17 : 101). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الإسرَاء Aya 111
Sura · الإسرَاء
Kiswahili · Barawani
17 : 101

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَىٰ تِسۡعَ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖۖ فَسۡـَٔلۡ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِذۡ جَآءَهُمۡ فَقَالَ لَهُۥ فِرۡعَوۡنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَٰمُوسَىٰ مَسۡحُورٗا

Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa!.

Explanation & meanings · 1
  1. Na lau hawa watu wangeli letewa hizo ishara wazitakazo, wange zigeuzia uso, wala wasinge ziamini! Na Sisi tulimpa Musa Ishara tisa wazi. Na juu ya hivyo wakakufuru. Na Firauni akasema: Hakika mimi nakuona wewe, Musa, ni mtu uliye rogwa! Hizo ishara tisa ni: 1. Fimbo, 2. Mkono Mweupe, 3. Tufani, 4. Nzige na vyura na chawa na damu, 5. Ukame na upungufu wa mazao, 6. Kupasuka bahari, 7. Kutimbuka maji baharini, 8. Kuning'inia mlima kama kivuli, 9. Kusemezwa na Mola wake Mlezi.