Skip to content
الإسرَاء /

Aya 102

17 : 102
الإسرَاء Aya 111
Sura · الإسرَاء
Kiswahili · Barawani
17 : 102

قَالَ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَآ أَنزَلَ هَٰٓؤُلَآءِ إِلَّا رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ بَصَآئِرَ وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَٰفِرۡعَوۡنُ مَثۡبُورٗا

Musa akasema: Wewe unajua bila ya shaka kuwa haya hakuyateremsha ila Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili kuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa umekwisha angamia.

Explanation & meanings · 1
  1. Musa akasema: Ewe Firauni! Unajua vyema kuwa aliye ziteremsha Ishara hizi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Kwani ni Yeye ndiye Mwenye kuweza hayo. Nazo Ishara hizo zi wazi, zinakuonyesha ukweli wangu. Lakini wewe unafanya kiburi na inadi tu. Na hakika mimi nakuona wewe, Firauni, kuwa ni mwenye kuangamia ikiwa hutoacha inadi yako.