Skip to content
إبراهِيم /

Aya 21

14 : 21

Aya 21 of إبراهِيم (14 : 21). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

إبراهِيم Aya 52
Sura · إبراهِيم
Kiswahili · Barawani
14 : 21

وَبَرَزُواْ لِلَّهِ جَمِيعٗا فَقَالَ ٱلضُّعَفَٰٓؤُاْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُوٓاْ إِنَّا كُنَّا لَكُمۡ تَبَعٗا فَهَلۡ أَنتُم مُّغۡنُونَ عَنَّا مِنۡ عَذَابِ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۚ قَالُواْ لَوۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ لَهَدَيۡنَٰكُمۡۖ سَوَآءٌ عَلَيۡنَآ أَجَزِعۡنَآ أَمۡ صَبَرۡنَا مَا لَنَا مِن مَّحِيصٖ

Na wote watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu. Wanyonge watawaambia walio takabari: Sisi tulikuwa wafwasi wenu; basi hebu hamtuondolei kidogo hivi katika adhabu ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Lau Mwenyezi Mungu angeli tuongoa basi hapana shaka nasi tungeli kuongoeni. Ni mamoja kwetu tukipapatika au tukisubiri; hatuna pa kukimbilia.

Explanation & meanings · 1
  1. Makafiri wote watadhihiri kutoka makaburini kwao, waonekane kwa ajili ya kuhisabiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kudhihiri huko hakuna shaka, ni kama kwamba yametokea hivi sasa. Hapo wale wenye maoni ya kinyonge miongoni mwa wafwasi watawaambia waongozi wenye kiburi: Sisi tulikuwa wafwasi wenu katika kuwakanusha Mitume na kuwapiga vita, na kuzipuuza nasaha zao. Basi je, hii leo, hamtuondolei kidogo baadhi ya adhabu? Wakubwa walio takabari watasema: Ingeli kuwa Mwenyezi Mungu ametuongoa kwenye njia ya kuokoka, na akatuwafikia, basi nasi tungeli kuongozeni na tungeli kuitieni muifuate hiyo njia. Walakini sisi tumepotea na kwa hivyo tukakupotezeni nyinyi, yaani tumekuchagulieni tuliyo jichagulia nafsi zetu. Na leo hii sisi na nyinyi ni sawa sawa, tukisikitika au tukastahamili. Hapana pa kuikimbilia adhabu hii!