Skip to content
هُود /

Aya 40

11 : 40

Aya 40 of هُود (11 : 40). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 40

حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَمۡرُنَا وَفَارَ ٱلتَّنُّورُ قُلۡنَا ٱحۡمِلۡ فِيهَا مِن كُلّٖ زَوۡجَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِ وَأَهۡلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيۡهِ ٱلۡقَوۡلُ وَمَنۡ ءَامَنَۚ وَمَآ ءَامَنَ مَعَهُۥٓ إِلَّا قَلِيلٞ

Hata ilipo kuja amri yetu, na tanuri ikafoka maji, tulisema: Pakia humo wawili wawili, dume na jike, kutoka kila aina, na ahali zako, isipo kuwa wale ambao imekwisha wapitia hukumu; na watu walio amini. Na hawakuamini pamoja naye ila wachache tu.

Explanation & meanings · 1
  1. Hata ulipo wadia wakati wa amri yetu ya kuwahilikisha, yalikuja maji kwa nguvu yakifoka na kutoa mapovu, kama maji yanavyo tokota juu ya moto. Tukamwambia Nuhu: Wapakie nawe katika hiyo Safina kutoka kila namna ya wanyama dume na jike. Na pia wapakie humo ahali zako, yaani watu wa nyumbani kwako, isipokuwa ilio kwisha pita juu yake hukumu yetu ya kumteketeza. Na pia kadhaalika wapakie humo katika watu wako walio amini. Na hao hawakuwa ila idadi chache tu.