Skip to content
هُود /

Aya 41

11 : 41

Aya 41 of هُود (11 : 41). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 41

۞ وَقَالَ ٱرۡكَبُواْ فِيهَا بِسۡمِ ٱللَّهِ مَجۡر۪ىٰهَا وَمُرۡسَىٰهَآۚ إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na akasema: Pandeni humo kwa Bismillahi, Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na baada ya kwisha liweka tayari jahazi Nuhu aliwaambia watu wake: Pandeni humo kwa kujipigia feli njema kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu (kupiga BISMILLAHI) wakati wa kwenda na wakati wa kusimama, na wakati wa kuingia na wakati wa kutoka humo. Na muombeni Mwenyezi Mungu akusameheni kwa madhambi mlio tenda, na akurehemuni. Kwani maghfira na rehema ni katika shani yake Subhanahu wa Taa'la.