Skip to content
هُود /

Aya 118

11 : 118

Aya 118 of هُود (11 : 118). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 118

وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ ٱلنَّاسَ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخۡتَلِفِينَ

Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana,.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Lau kuwa Mola wako Mlezi angeli penda angeli wafanya watu wote wafuate Dini moja, wakimt'ii Mwenyezi Mungu kwa ut'iifu wa maumbile, kama Malaika. Na ulimwengu ungeli kuwa sio ulimwengu huu. Lakini Yeye Subhanahu hakutaka hayo, bali amewaacha waweze kuchagua wenyewe. Basi hawaachi kukhitalifiana katika kila kitu, hata katika misingi ya imani, kama kumuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho - mambo ambayo haifai kukhitalifiana kwayo. Wao hufuata nyoyo zao, na matamanio yao, na fikra zao, kila kikundi kimeshikilia kwa nguvu rai ile ile walio kutana nayo kwa baba zao!