11 : 117
وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهۡلِكَ ٱلۡقُرَىٰ بِظُلۡمٖ وَأَهۡلُهَا مُصۡلِحُونَ
Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema.
Explanation & meanings · 1
- Wala sio mwendo wake Mwenyezi Mungu, wala sio uadilifu wake wa maumbile, kuudhulumu umma wowote akauteketeza nao unashikamana na Haki, unafuata mwendo bora, unatenda yanao wafaa wao na wenginewe.