Skip to content
هُود /

Aya 10

11 : 10

Aya 10 of هُود (11 : 10). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 10

وَلَئِنۡ أَذَقۡنَٰهُ نَعۡمَآءَ بَعۡدَ ضَرَّآءَ مَسَّتۡهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ ٱلسَّيِّـَٔاتُ عَنِّيٓۚ إِنَّهُۥ لَفَرِحٞ فَخُورٌ

Na tukimwonjesha neema baada ya madhara yaliyo mpata husema: Taabu zimekwisha niondokea. Hakika yeye hujitapa na kutafakhari.

Explanation & meanings · 1
  1. Na tukimpa neema baada ya shida aliyo kuwa nayo yeye husema: Shida zangu zote zimekwisha niondokea, wala hazitarudi tena! Na hayo humpelekea upeo wa kufurahikia starehe za dunia, na kujifakhirisha bila ya kiasi. Moyo wake huwa umeshughulika, usimshukuru Mola wake Mlezi! Hii ndiyo hali ya binaadamu wengi, wanababaika baina ya kukata tamaa na kujitapa!