Skip to content
يُونس /

Aya 64

10 : 64

Aya 64 of يُونس (10 : 64). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 64

لَهُمُ ٱلۡبُشۡرَىٰ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۚ لَا تَبۡدِيلَ لِكَلِمَٰتِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hapana mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Kwa wapenzi hawa wa Mwenyezi Mungu pana bishara ya kheri hapa duniani, kwa vile Mwenyezi Mungu amewaahidi kuwapa ushindi na utukufu, na Akhera itatimia ahadi ya Mwenyezi Mungu. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu haigeuki. Na haya ndiyo waliyo bashiriwa kwayo duniani, na watayapata Akhera. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.