Skip to content
يُونس /

Aya 65

10 : 65
يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 65

وَلَا يَحۡزُنكَ قَوۡلُهُمۡۘ إِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًاۚ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Wala yasikuhuzunishe maneno yao. Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Mtume! Usihuzunuke kwa wayasemayo washirikina ya kejeli, na matusi, na kukadhibisha. Wala usidhani kuwa hali yao hii itadumu. Bali ushindi ni wako, na Uislamu utatukuka, kwani utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ushindi upo mkononi mwake, na Yeye atakunusuru uwashinde hao makafiri. Na Yeye Subhanahu ni Mwenye kuyasikia wanayo kuzulia, na Mwenye kuyajua wanayo dhamiria. Na Yeye atawalipa kwa hayo.