Skip to content
يُونس /

Aya 59

10 : 59

Aya 59 of يُونس (10 : 59). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 59

قُلۡ أَرَءَيۡتُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ لَكُم مِّن رِّزۡقٖ فَجَعَلۡتُم مِّنۡهُ حَرَامٗا وَحَلَٰلٗا قُلۡ ءَآللَّهُ أَذِنَ لَكُمۡۖ أَمۡ عَلَى ٱللَّهِ تَفۡتَرُونَ

Sema: je, mwaonaje zile rizki alizo kutemshieni Mwenyezi Mungu nanyi makafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali Sema: je, Mwenyezi Mungu amekuruhusuni au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Mtume! Waambie makafiri walio pewa baadhi ya starehe za duniani: Niambieni khabari ya vyakula vizuri vya halali alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, mkajifanya wenyewe ni watungaji sharia, mkahalalisha vingine na mkaharimisha vingine, bila ya kufuata Sharia ya Mwenyezi Mungu! Hakika Mwenyezi Mungu hakukupeni ruhusa mfanye hayo, bali nyinyi mnamzulia uwongo Mwenyezi Mungu.