Skip to content
يُونس /

Aya 47

10 : 47

Aya 47 of يُونس (10 : 47). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 47

وَلِكُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولٞۖ فَإِذَا جَآءَ رَسُولُهُمۡ قُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Na kila umma ulijiwa na Mtume akafikisha wito wa Mwenyezi Mungu, akaamini aliye amini, na akakanusha aliye kanusha. Ikifika Siku ya kufufuliwa, Mtume wao atakuja na kuwatolea ushahidi wale walio mkadhibisha kuwa hao ni makafiri, na walio amini kuwa ni Waumini. Basi Mwenyezi Mungu atawahukumu kwa uadilifu ulio timia. Hatomdhulumu yeyote katika malipo anayo stahiki.