Skip to content
يُونس /

Aya 36

10 : 36

Aya 36 of يُونس (10 : 36). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 36

وَمَا يَتَّبِعُ أَكۡثَرُهُمۡ إِلَّا ظَنًّاۚ إِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا يَفۡعَلُونَ

Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Na dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika Mwenyezi Mungu anajua yote wanayo yatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Wengi wa washirikina hawafuati katika itikadi zao ila dhana potovu zisio kuwa na dalili zozote! Na kwa jumla, dhana haifidi kitu, wala haiwezi kuwa ni badala ya kuijua Haki, na khasa ikiwa dhana yenyewe ni ya kuzua tu, kama hizi dhana za washirikina. Na hakika Mwenyezi Mungu anayajua vyema wayafanyayo wakuu wa ukafiri na wafuasi wao, naye atawalipa kwa hayo.