Skip to content
يُونس /

Aya 34

10 : 34

Aya 34 of يُونس (10 : 34). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 34

قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۚ قُلِ ٱللَّهُ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ

Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina aliye anzisha kuumba viumbe, na kisha akavirejesha? Huwaje, basi, mkadanganywa?

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Mtume! Waambie hao washirikina: Yupo yeyote katika hao mlio wafanya washirika wa Mwenyezi Mungu mkawaabudu, awezaye kuanzisha kuumba tangu mwanzo, na tena akarejea tena baada ya kwisha toweka? Hapana shaka watashindwa kujibu! Basi hapo tena waambie: Allah, Mwenyezi Mungu, tu peke yake, ndiye anaye anzisha kuumba kutokana na kuto kuwepo, na tena viumbe vikitoweka huvirejesha. Vipi basi nyinyi mnaiacha Imani?