Skip to content
يُونس /

Aya 26

10 : 26

Aya 26 of يُونس (10 : 26). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 26

۞ لِّلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ ٱلۡحُسۡنَىٰ وَزِيَادَةٞۖ وَلَا يَرۡهَقُ وُجُوهَهُمۡ قَتَرٞ وَلَا ذِلَّةٌۚ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila. Hao ndio watu wa Peponi. Humo watadumu.

Explanation & meanings · 1
  1. Wanao tenda mema kwa kuitikia Wito wa Mwenyezi Mungu, wakaamini na wakafanya kheri kwa Dini yao na dunia yao, hao watapata wema katika Akhera, na wema huo ni Pepo. Na tena watapata yaliyo zidi hayo kwa fadhila na ukarimu wa Mwenyezi Mungu. Wala nyuso zao hazitafunikwa na huzuni na hamu na fedheha. Hawa ndio watu wa Peponi watakao neemeka humo daima milele.