10 : 25
وَٱللَّهُ يَدۡعُوٓاْ إِلَىٰ دَارِ ٱلسَّلَٰمِ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ
Na Mwenyezi Mungu anaita kwendea Nyumba ya Amani, na anamwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka.
Explanation & meanings · 1
- Na Mwenyezi Mungu anawaitia waja wake kwa Imani na vitendo vyema wendee Peponi, makao ya amani na utulivu. Na Yeye Subhanahu humwongoa amtakaye - kwa kuwa kesha jitayarisha vyema na kaelekea kheri - kwenye Njia ya Haki, nayo ni ya Salama.