Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 4 kati ya 839

Ondoa vichujio

Daraja la hadithi

Yakwamba mtu wa kijijini alimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mungu na wala usimshirikishe na chochote, na usimamishe swala na utoe zaka ya wajibu, na ufunge mwezi wa ramadhani" Akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, sitozidisha zaidi ya hapo, basi alipoondoka, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayependezwa na kumtazama mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame huyu".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, huenda mfikishiwa akawa mwerevu zaidi kuliko aliye sikia".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa kwa ajili ya kupata masilahi ya kidunia, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama" Yaani: Upepo yake.
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? Akasema: "Basi semeni: Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammadi na juu ya watu wa Muhammadi, kama ulivyompa rehema Ibrahim na juu ya watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa, ewe Mwenyezi Mungu shusha baraka juu ya Muhammad na juu ya watu wa Muhammad, kama ulivyoteremsha baraka kwa watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake