Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiyekuwa na mshirika, Mwenyezi Mungu mkubwa mno, na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu mwenye nguvu na hekima
Kutoka kwa Sa'di radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alikuja bedui kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: Nifundishe maneno nitakayoyasema. Akasema "Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiyekuwa na mshirika, Mwenyezi Mungu mkubwa mno, na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu mwenye nguvu na hekima" Akasema: Haya ni kwa ajili ya Mola wangu, yako wapi ya kwangu? Akasema: "Sema: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi na unihurumie na uniongoze na uniruzuku".
جَاءَ أَعْرَابِيٌّ إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: عَلِّمْنِي كَلَامًا أَقُولُهُ، قَالَ: «قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، اللهُ أَكْبَرُ كَبِيرًا، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثِيرًا، سُبْحَانَ اللهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ، لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ» قَالَ: فَهَؤُلَاءِ لِرَبِّي، فَمَا لِي؟ قَالَ: «قُلْ: اللهُمَّ اغْفِرْ لِي وَارْحَمْنِي وَاهْدِنِي وَارْزُقْنِي».
Mtu mmoja miongoni mwa watu wa kijijini alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amfundishe dhikiri atakayokuwa akiisema, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Sema: "Laa ilaaha illa llaah wahdahu laa shariika lahu" (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake) Ameanza kwa shahada ya tauhidi, na maana yake hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, "Allaahu Akbaru kabiira" Yaani: Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko kila kitu na ni Mtukufu, "Na Alhamdulillaahi kathira" Yaani: Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu kwa wingi, kwa sifa zake na vitendo vyake na neema zake zisizohesabika, "Sub-haanallaahi rabbil Aalamiin" Yaani: Ametukuka na kutakasika na kila mapungufu, "Laa haulaa walaa quwwata illaa billaahil Azizil Hakiim" Yaani: Hakuna namna ya kugeuka kutoka hali moja kwenda hali nyingine isipokuwa kwa uweza wa Allah na msaada wake na taufiki yake, Yule bwana akasema: Maneno haya ni kwa ajili ya Mola wangu Mlezi, kwa kumtaja yeye na kumtukuza, ya kwangu mimi ya kujiombea mwenyewe yako wapi? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Sema: "Ewe Mola wangu nisamehe" Kwa kuyafuta madhambi na kuyasitiri, "Na unihurumie" Kwa kuniletea manufaa na masilahi ya dini na dunia kwangu, "Na uniongoze" Kwenda katika hali nzuri na katika njia iliyonyooka, "Na uniruzuku" Mali ya halali na siha na kila aina ya kheri na afya.
...:
Kuna himizo la kumtaja Mwenyezi Mungu kwa neno 'Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbar, na Alhamdulillaah, na Sub-haanallaah.
Ni sunna kumtaja Mwenyezi Mungu na kumsifu kabla ya kumuomba.
Ni suuna mtu kuomba kwa dua nzuri, na kwa dua zilizopokelewa toka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, ambazo zimekusanya kila aina ya kheri za Dunia na Akhera, na ana uhuru wa kuomba akitakacho.
Inampasa mja apupie kujifunza yale yenye kumnufaisha katika Dunia na Akhera.
Himizo la kuomba msamaha na huruma na riziki, kwani mambo haya yamekusanya kheri zote.
Huruma yake rehema na amani ziwe juu yake katika kuufundisha umma wake yale yenye kuwanufaisha.
Imetajwa huruma baada ya msamaha ili usafi ukamilike,na msamaha ni kusitiriwa makosa na kufutwa kwake na kuepushwa na moto, na huruma ni kufikishiwa kheri na kuingia peponi, na huku ndiko kufaulu kukubwa.
Swahiih Muslim (4/ 2072) (2696).
Zaidi (6)
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.
لسليم الهلالي (2/ 498).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.
لمجموعة من الباحثين (2/ 972).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح.
لعلي القاري (4/ 1606).
Imenukuliwa katika vitabu
11 Vitabu- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلم"Hakuna uwezo wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu."[44]
- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلمLaa haula walaa kuwwata illaa billah
- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلم(Hakuna uwezo wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu)."[306]
- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلمLaa haula walaa kuwwata illaa billaah
- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلم"Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Yeye pekee asiyekuwa na mshirika, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa mno, na kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na h
- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلمLa ilaha illallahu wahdahu la sharika lahu, Allahu akbaru kabira, walhamdu lillahi kathira, subhanallahi rabbil alamin, la hawla wala quwwata illa billahil azizil hakim.
Zaidi (5)
- الذكر والدعاء والعلاج بالرقي من الكتاب والسنة"قل: لا إله إلا الله وحده لا شريك له، الله أكبر كبيراً والحمدُ لله كثيراً، سبحان الله رب العالمين، لا حول ولا قوة إلا بالله العزيز الحكيم" قال فهؤلاء لربي فمالي؟ قال "قل: اللهم اغفر لي، وارحمني، واهدني وارزقني".
- المختصر المفيد للمؤذن والإمام والخطيب وأحكام المساجد«لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ»
- تحفة الأخيار تحفة الأخيار (ببيان جملة نافعة مما ورد في الكتاب والسنة من الأدعية والأذكار)«قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيرًا، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثِيرًا، سُبْحَانَ اللَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ، لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ» قَالَ: فَهَؤُلَاءِ لِرَ
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 7«قُل: لا إلهَ إلَّا اللهُ وحدَهُ لا شريكَ لَهُ، اللهُ أكبرُ كبيراً، والحمدُ لله كثيراً، وَسُبْحَانَ اللهِ ربِّ العالمين، ولا حولَ ولا قوَّةَ إلَّا بالله العزيزِ الحكيمِ» قَالَ: فهؤلاء لربِّي، فما لي؟ قَالَ: «قُل: اللّهم اغفرْ لي، وارحمْني،
- فضل الدعاء وآدابه والأوقات التي يستحب فيها"لا حول ولا قوة إلا بالله"