Skip to content

Hakika waadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika mimbari za nuru, kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake yote miwili ni kulia

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:

"Hakika waadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika mimbari za nuru, kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake yote miwili ni kulia , wale wanaofanya uadilifu katika hukumu zao na familia zao, na vile wanavyovitawala"

«إِنَّ الْمُقْسِطِينَ عِنْدَ اللهِ عَلَى مَنَابِرَ مِنْ نُورٍ، عَنْ يَمِينِ الرَّحْمَنِ عَزَّ وَجَلَّ، وَكِلْتَا يَدَيْهِ يَمِينٌ، الَّذِينَ يَعْدِلُونَ فِي حُكْمِهِمْ وَأَهْلِيهِمْ وَمَا وَلُوا».

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wanaohukumu kwa uadilifu na haki baina ya watu walio chini ya utawala wao na hukumu zao, na familia zao, nikuwa watakaa katika makao ya juu zaidi yaliyoumbwa kwa nuru, ikiwa ni takrima kwao siku ya Kiyama. Na mimbari hizi ziko kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake miwili Mtukufu yote ni kulia.

Maana ya Maneno

المقسطين: العادلين.

في حكمهم: في قضائهم.

ما وَلُوا: الذي كانت لهم عليه ولاية.

Katika Faida za Hadithi

Fadhila za uadilifu na himizo juu yake.

Uadilifu ni neno la kiujumla linalokusanya tawala zote, na hukumu za kati ya watu hata uadilifu kati ya wake na watoto, na mengineyo.

Kumebainishwa nafasi ya waadilifu siku ya Kiyama.

Kutofautiana kwa makazi ya watu wa imani siku Kiyama kila mmoja atakuwa kulingana na matendo yake.

Mfumo wa kuhamasisha ni katika njia za kufanya da'wa zinazomvutia mwenye kulinganiwa kuja katika utiifu.

Rejea

Swahiih Muslim (3/ 1458) (1827).

Zaidi (10)

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (1/ 547).

تطريز رياض الصالحين.

لفيصل المبارك (ص428).

كنوز رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (9/ 314).

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (1/ 710).

شرح رياض الصالحين.

لابن عثيمين (3/ 640).