Skip to content

Sikuacha baada yangu fitina yenye madhara zaidi kwa wanaume kuliko wanawake

Kutoka kwa Osama bin Zaidi -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

"Sikuacha baada yangu fitina yenye madhara zaidi kwa wanaume kuliko wanawake".

«مَا تَرَكْتُ بَعْدِي فِتْنَةً أَضَرَّ عَلَى الرِّجَالِ مِنَ النِّسَاءِ».

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuacha baada yake majaribu na mtihani wenye madhara makubwa kwa wanaume kuliko wanawake; Mwanamke akiwa ni katika familia yake huenda mume akamfuata mwanamke katika kwenda kinyume na sheria, na akiwa ni mwanamke wa kando yaweza kuwa ni kwa sababu ya kuchanganyika naye na kukaa naye faragha, na maovu mengine yanayoweza kusababishwa na hilo.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Ni lazima kwa muislamu kutahadhari na fitina ya wanawake, na kuziba njia zote zinazopelekea kufitinika nao.

Ni lazima kwa muumini ashikamane na Mwenyezi Mungu, na kujiweka karibu naye katika kutaka kusalimika na fitina.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (7/ 8) (5096).

Swahiih Muslim (4/ 2097) (2740).

Zaidi (3)

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (373).

فتح الباري لابن حجر (9/ 138).