Skip to content

Alikataza kula kila chenye meno ya chonge katika wanyama wanaoshambulia, na kila chenye mdomo wa chonge katika ndege

Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake -:

Alikataza kula kila chenye meno ya chonge katika wanyama wanaoshambulia, na kila chenye mdomo wa chonge katika ndege.

نَهَى عَنْ كُلِّ ذِي نَابٍ مِنَ السِّبَاعِ، وَعَنْ كُلِّ ذِي مِخْلَبٍ مِنَ الطَّيْرِ.

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Alikataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kula kila chenye kuwinda katika wanyama wenye kushambulia, kinachowinda kwa meno ya mbele, na akakataza kula kila ndege anayekata na kukamata kwa mdomo wake.

Katika Faida za Hadithi

Pupa ya Uislamu juu ya vitu vizuri katika kila kitu miongoni mwa vyakula na vinywaji na vinginevyo.

Asili katika vyakula ni uhalali; isipokuwa vile vilivyoelezwa na sheria kuwa ni haram.

Rejea

Swahiih Muslim (3/ 1534) (1934).

Zaidi (9)

سبل السلام شرح بلوغ المرام.

للصنعاني (2/ 506).

توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام.

لعبد الله البسام (7/ 5).

فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام.

لابن عثيمين (6/ 6).

منحة العلام في شرح بلوغ المرام.

لعبد الله الفوزان (9/ 173).

فتاوى اللجنة الدائمة - المجموعة الأولى (22/ 290).