Skip to content

Hakika ninachokiogopea zaidi juu yenu ni shirki ndogo" Wakasema: Ni ipi shirki ndogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni riyaa (kujionyesha)

Imepokelewa kutoka kwa Mahmud bin Labid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

"Hakika ninachokiogopea zaidi juu yenu ni shirki ndogo" Wakasema: Ni ipi shirki ndogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni riyaa (kujionyesha), atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama kuwaambia, pindi watu wote watakapolipwa kwa matendo yao: 'Nendeni kwa wale mliokuwa mkijionyesha kwao duniani, mtazame je mtapata kwao malipo?".

«إِنَّ أَخْوَفَ مَا أَخَافُ عَلَيْكُمُ الشِّرْكُ الْأَصْغَرُ» قَالُوا: وَمَا الشِّرْكُ الْأَصْغَرُ يَا رَسُولَ اللهِ؟ قَالَ: «الرِّيَاءُ، يَقُولُ اللهُ عز وجل لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِذَا جُزِيَ النَّاسُ بِأَعْمَالِهِمْ: اذْهَبُوا إِلَى الَّذِينَ كُنْتُمْ تُرَاؤُونَ فِي الدُّنْيَا، فَانْظُرُوا هَلْ تَجِدُونَ عِنْدَهُمْ جَزَاءً؟».

Imepokelewa na Ahmad
Ni nzuri (Hasan)
Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa jambo kubwa zaidi analoliogopea juu ya umma wake: Ni shirki ndogo nayo; ni mtu kufanya kwa ajili ya watu. Kisha akaeleza kuhusu adhabu ya wenye kujionyesha siku ya Kiyama kwa kuambiwa: Nendeni kwa wale mliokuwa mkifanya kwa ajili yao, mkatazame je wanamiliki malipo na thawabu za kukupeni kwa amali hiyo?!.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Ulazima wa kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutahadhari na riyaa.

Huruma yake kubwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya umma wake na pupa yake ya kutaka kuwaongoza na kuwapa kwake nasaha.

Ikiwa hii ndio hofu yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akizungumza na Masahaba ambao ndio watukufu kwa watu wema, basi hofu kwa wale wataokuja baada yao ni kubwa zaidi.

Rejea

Musnad wa Ahmad (39/ 39) (23630).

Zaidi (4)

الجديد في شرح كتاب التوحيد.

لمحمد القرعاوي (ص57).

الملخص في شرح كتاب التوحيد.

لصالح الفوزان (ص45).