Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu".
«لَا يَحِلُّ لِرَجُلٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلَاثِ لَيَالٍ، يَلْتَقِيَانِ، فَيُعْرِضُ هَذَا وَيُعْرِضُ هَذَا، وَخَيْرُهُمَا الَّذِي يَبْدَأُ بِالسَّلَامِ».
Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu kumhama ndugu yake muislamu zaidi ya siku tatu, wanakutana wote hamsalimii wala hamsemeshi. Na mbora kati ya hawa wagomvi wawili ni yule anayejaribu kuondoa kuhamana huku, na akaanza kwa salamu, na makusudio ya kuhamana hapa ni sababu ya kujikweza, ama kuhamana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama kuwahama waovu na wazushi na marafiki waovu, hili halina muda maalum, bali limeambatana na masilahi katika kuhama, na linamalizika kwa kuondoka maslilahi yake.
...:
Uhalali wa kumhama mtu ndani ya siku tatu kurudi chini, kwa kulinda maumbile ya kibinadamu, itasamehewa ndani ya siku tatu, ili kiondoke kile kilichojitokeza baina yao.
Ubora wa salamu, nakuwa huondoa yaliyoko ndani ya nafsi, nakuwa ni alama ya kupendana.
Pupa ya Uislamu juu ya udugu na ukaribu baina waislamu.
Swahiih Al Bukhaariy (8/ 21) (6077).
Swahiih Muslim (4/ 1984) (2560).
Zaidi (6)
منحة العلام في شرح بلوغ المرام.
لعبد الله الفوزان (10/ 111).
فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام.
لابن عثيمين (6/ 293).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام.
للبسام (7/ 339).
Imenukuliwa katika vitabu
2 VitabuZaidi (2)
- المناهج التعليمية - الصف السادسالمناهج الدراسية - الحديث - الصف السادس - الفصل الأول «لَا يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلَاثِ لَيَالٍ، يَلْتَقِيَانِ فَيُعْرِضُ هَذَا وَيُعْرِضُ هَذَا، وَخَيْرُهُمَا الَّذِي يَبْدَأُ بِالسَّلَامِ»
- المناهج التعليمية - الصف السادسالمناهج الدراسية - الحديث - الصف السادس - الفصل الأول «وخَيْرُهُما الذي يَبْدَأ بِالسَّلَامِ».