alikuwa anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake mkarimu, na kwa mamlaka yake ya tangu, kutokana na shetani aliyelaaniwa
Kutoka kwa Abdallahi bin Amru bin A'swi -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake:
Kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yakwamba yeye alikuwa anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake mkarimu, na kwa mamlaka yake ya tangu, kutokana na shetani aliyelaaniwa" Akasema: Hivyo tu? Nikasema ndiyo. Akasema: Mtu anaposema hivyo shetani husema: Huyu kalindwa nami siku yake nzima.
عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه كان إذا دخل المسجد قال: «أعوذ بالله العظيم، وبوجهه الكريم، وسلطانه القديم، من الشيطان الرَّجِيم»، قال: أَقَطُّ؟ قلت: نعم، قال: فإذا قال ذلك قال الشيطان: حُفِظَ منِّي سائر اليوم.
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu" Yaani: Ninashikamana na kuegemea kwa Mwenyezi Mungu na sifa zake. "Na kwa uso wake Mkarimu" Yaani: Mkarim mtoaji, "Na kwa mamlaka yake) Yaani: Ushindi wake na uweza wake kwa amtakaye katika viumbe wake "Wa tangu" Yaani: Wa zamani na wa milele. "Kutokana na Shetani aliyelaaniwa" Yaani: Aliyetengwa na kufukuzwa kutoka katika rehema ya Mwenyezi Mungu, yaani: Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi kutokana na wasi wasi wake na upotoshaji wake na hatua zake na hatari zake, na udanganyifu wake na upotoshaji wake, kwani yeye ndiye sababu ya upotofu, na ndio mchochezi wa upotofu na ujinga, akaulizwa Abdillah bin Amri "Hivyo tu" Yaani: Je, alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni hivyo tu? Akasema: Ndio. Atakaposema dua hii mwenye kuingia msikitini; Shetani husema: Muingiaji kaihifadhi nafsi yake dhidi yangu wakati wake wote, mchana wake na usiku wake.
Fadhila za kuomba kwa dua hii wakati wa kuingia msikitini, nakuwa dua hii humkinga msemaji wake kutokana na Shetani siku nzima.
Tahadhari kutokana na Shetani, nakuwa humuwinda Muislamu; kwa ajili ya kumpoteza na kumshawishi.
Mtu atalindwa kutokana na upotofu na udanganyifu wa Shetani kwa kiwango ambacho moyo wake unamwamini Mwenyezi Mungu na kuihudhurisha dua hii, na kuamini kwake ahadi za Mwenyezi Mungu zinazotokana nayo.
Sunanu Abii Daud (1/ 349) (466).
Zaidi (4)
شرح سنن أبي داود.
لبدر الدين العيني (2/ 374).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح.
لعلي القاري (2/ 627).
Imenukuliwa katika vitabu
9 Vitabu- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلم"Ninajilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake Mkarimu, na kwa ufalme wake wa enzi, kutokana na shetani aliyelaaniwa."[38]
- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلمAudhu billahil adhiim, wa bi wajhihil kariim, wa sultanihil qadiim, minash shaitanir rajiim.
- Fadhila na adabu za Msikiti wa bwana Mtume na hukumu za kuzuru kaburi la Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kaburi za Maswahaba zake wawili, Mwenyezi Mungu awe radhi naoفضائل وآداب المسجد النبوي، وأحكام زيارة قبر النبي عليه الصلاة والسلام وقبري صاحبيه"Ninajilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake Mkarimu, na kwa ufalme wake wa enzi, kutokana na shetani aliye laaniwa."[10]
Zaidi (6)
- الذكر والدعاء والعلاج بالرقي من الكتاب والسنة"أعوذ بالله العظيم، وبوجهه الكريم، وسلطانه القديم من الشيطان الرجيم -فإذا قال ذلك قال الشيطان: حُفِظَ مني سائر اليوم".
- الصلاة التي علمها النبي ﷺ الصحابة رضي الله عنهمالصلاة التي علمها النبي ﷺ الصحابة رضي الله عنهم«أعوذُ باللهِ العظيمِ، وبوجهِهِ الكريم، وسُلطانِه القديم، من الشَّيطانِ الرَّجيم» قال: أَقَطْ؟ قلتُ: نعم، قال: «فإذا قالَ ذلك قالَ الشَّيطانُ: حُفِظَ منِّي سائرَ اليَومِ»[121].
- الصلاة التي علمها النبي ﷺ الصحابة رضي الله عنهم«أَعُوذُ بِاللَّهِ العَظِيمِ، وَبِوَجْهِهِ الكَرِيمِ، وَسُلْطَانِهِ القَدِيمِ، مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ» قَالَ: أَقَطْ؟ قُلْتُ: نَعَمْ، قَالَ: «فَإِذَا قَالَ ذَلِكَ قَالَ الشَّيْطَانُ: حُفِظَ مِنِّي سَائِرَ اليَوْمِ»[121].
- تحفة الأخيار تحفة الأخيار (ببيان جملة نافعة مما ورد في الكتاب والسنة من الأدعية والأذكار)«أَعُوذُ بِاللَّهِ الْعَظِيمِ، وَبِوَجْهِهِ الْكَرِيمِ، وَسُلْطَانِهِ الْقَدِيمِ، مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ، قَالَ: «فَإِذَا قَالَ: ذَلِكَ قَالَ الشَّيْطَانُ: حُفِظَ مِنِّي سَائِرَ الْيَوْمِ» [61]
- رسالة في الأذكار1«أَعُوذُ بِاللهِ الْعَظِيمِ، وَبِوَجْهِهِ الْكَرِيمِ، وَسُلْطَانِهِ الْقَدِيمِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ». قال: «فَإِذَا قَالَ ذَلِكَ قَالَ الشَّيْطَانُ: حُفِظَ مِنِّي سَائِرَ الْيَوْمِ».
- مجموعة زاد التربية الإسلامية (3)، والسيرة النبوية (3)التربية الإٍسلامية -3- «أعوذُ باﷲِ العظيمِ، وبوجهِهِ الكريمِ، وسُلطانِهِ القديمِ، من الشَّيطانِ الرَّجيم»