Skip to content
الأنفَال /

Aya 48

8 : 48

Aya 48 of الأنفَال (8 : 48). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنفَال Aya 75
Sura · الأنفَال
Kiswahili · Barawani
8 : 48

وَإِذۡ زَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ ٱلۡيَوۡمَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَإِنِّي جَارٞ لَّكُمۡۖ فَلَمَّا تَرَآءَتِ ٱلۡفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِ وَقَالَ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّنكُمۡ إِنِّيٓ أَرَىٰ مَا لَا تَرَوۡنَ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَۚ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Na pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao, na akawaambia: Hapana watu wa kukushindeni hii leo, na hali mimi ni mlinzi wenu. Yalipo onana majeshi mawili, akarudi nyuma, na akasema: Mimi si pamoja nanyi. Mimi naona msiyo yaona. Mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na kumbukeni, enyi Waislamu! Pale Shetani alipo kuja kuwazaini hawa washirikina kwa kuwaonyesha kuwa wayatendayo ni mazuri kwa uchochezi wake, akiwaambia: Hapana mtu ye yote anaye weza kuwashinda. Na akawahakikishia kuwa yeye atawalinda, na kuwanusuru! Yalipo kutana makundi mawili katika vita, vitimbi vyake na uchochezi wake ukavunjika. Akarejea nyuma, na akajitoa nao, akaogopa Mwenyezi Mungu asimuangamize. Na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.