Skip to content
Al-Anfal /

Aya 49

8 : 49

Aya 49 of Al-Anfal (8 : 49). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-Anfal Aya 75
Sura · Al-Anfal
Kiswahili · Barawani
8 : 49

إِذۡ يَقُولُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ غَرَّ هَٰٓؤُلَآءِ دِينُهُمۡۗ وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Na walipo sema wanaafiki, na wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao: Watu hawa dini yao imewadanganya. Na Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Ametukuka, na Mwenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Na kumbuka ewe Mtume! Walipo sema wanaafiki miongoni mwa makafiri na wale wenye Imani dhaifu walipo kuoneni mmesimama imara: Hawa Waislamu wameghurika kweli na dini yao! Na hakika mwenye kumwakilisha Mwenyezi Mungu jambo lake, na akamuamini Yeye, na akamtegemea Yeye, basi hapana shaka kuwa Mwenyezi Mungu atamkifia amwondolee hamu yake, na atamnusuru na maadui zake. Kwani hakika Mwenyezi Mungu madaraka yake yana nguvu, naye ni Mwenye hikima katika mipango yake.