8 : 32
وَإِذۡ قَالُواْ ٱللَّهُمَّ إِن كَانَ هَٰذَا هُوَ ٱلۡحَقَّ مِنۡ عِندِكَ فَأَمۡطِرۡ عَلَيۡنَا حِجَارَةٗ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ أَوِ ٱئۡتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٖ
Na walipo sema: Ee Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ni kweli itokayo kwako basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tuletee adhabu yoyote iliyo chungu.
Explanation & meanings · 1
- Na kumbuka, ewe Nabii, vipi walivyo kuwa wanakupinga na kumpinga Mwenyezi Mungu hata kwa inda yao wakasema kumwambia Mwenyezi Mungu, Mola wao Mlezi: Ikiwa haya unayo kuja nayo ni mambo madhbuti, basi zijaalie mbingu zitunyeshee mawe, au tuletee adhabu yoyote iliyo kali yenye uchungu!