67 : 23
قُلۡ هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُمۡ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَۚ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ
Sema: Yeye ndiye aliye kuumbeni tangu mwanzo, na akakupeni masikio na macho, na nyoyo. Ni kidogo kabisa shukrani zenu.
Explanation & meanings · 1
- Sema: Huyo aliye kuumbeni nanyi hamjakuwa chochote, na akakupeni usikizi na kuona, na fahamu ambazo ni sababu za vitendo vyenu na uwongofu wenu - ama ni kuchache mno kushukuru kwenu kwa neema hizi kumshukuru huyo aliye kupeni.