63 : 8
يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعۡنَآ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ لَيُخۡرِجَنَّ ٱلۡأَعَزُّ مِنۡهَا ٱلۡأَذَلَّۚ وَلِلَّهِ ٱلۡعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِۦ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَعۡلَمُونَ
Wanasema: Tukirejea Madina mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza aliye mnyonge. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui.
Explanation & meanings · 1
- Wanaafiki wanasema kwa kutoa ahadi: Tukirejea Madina hapana shaka kikundi chetu, ambacho ndicho chenye nguvu zaidi, kitakitoa kikundi cha Waumini ambao ni wanyonge! Nguvu anazo Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini; sio hawa wanao jitia kuahidi. Lakini wanaafiki hawajui kitu.