Skip to content
الأنعَام /

Aya 73

6 : 73

Aya 73 of الأنعَام (6 : 73). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 73

وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۖ وَيَوۡمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُۚ قَوۡلُهُ ٱلۡحَقُّۚ وَلَهُ ٱلۡمُلۡكُ يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِۚ عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ

Naye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Na anaposema: Kuwa! Basi huwa. Kauli yake ni Haki. Na ufalme wote ni wake Siku litapo pulizwa barugumu, Mjuzi wa yaliyo fichikana na yanayo onekana. Naye ndiye Mwenye hikima na Mwenye khabari.

Explanation & meanings · 1
  1. Na ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akasimamia uumbaji wake kwa Haki na hikima. Na wakati wowote Mwenyezi Mungu akitaka kiwe kitu kinakuwa papo hapo. Vitu huwa kwa neno: "Kuwa". Na kila neno lake ni la kweli na la haki. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye uweza wa kutenda usio na ukomo Siku ya Kiyama, siku litapo pulizwa barugumu la kutangazwa ufufuo. Naye, Subhanahu, ndiye Mwenye kutulia juu ya ujuzi wake wa mambo yaliyo fichikana na yanayo onekana. Na ndiye anaye endesha mambo yake yote kwa hikima, na ndiye Mwenye kukusanya katika ujuzi wake mambo yaliyo fichikana na mambo yaliyo dhihiri.